Skip to content Skip to right sidebar Skip to footer

ANNOUNCEMENT

TANGAZO MUHIMU

Welcome to Samandito Primary School

Uongozi wa shule ya msingi Samandito unayofuraha kuwakaribisha na kuwatangazia nafasi za mwasomo kwa madarasa yote kuanzia chekechea hadi darasa la Saba.

Shule ina mazingira mazuri na tulivu ya kumfanya mwanao ajifunze na kuelewa. Mbali na mazingiza, shule hii pia inafanya vizuri katika mitihani ya ndani na nje ya shule.

Hii ni shule pekee katika mkoa wa geita itakayo mafanya mwanao aweze kuongea vizuri lugha ya kiingereza kulingana na msisitizo na ufuatiliaji mkubwa kati ya uongozi na waalimu pia.

Shule ina waalimu wenye maarifa na weledi wa hali ya juu ambao wako tayari kabisa kumfanya mwanao afikie malemgo yake ya maisha, sio waalimu wa kutimiza ratiba bali ni waalimu wanaofanya kazi kwa kujitoa ili kumfanya mwanao ainuke kitaaluma.

Ukitaka ushangae mabadiliko ya mwanao kitaaluma katika viwango vya juu usivyotarajia basi suluhu ni moja tu, mlete mwanao shule ya Samandito English Medium nawe siku moja utasimulia mabadiliko makubwa ya mwanao.

Shule hii inapatikana Mkoa wa Geita, wilaya ya Geita mjini, Kata ya Buhalahala, mkabala na shule ya Secondary Mwatulole.

Ada zetu ni nafuu sana na unaruhusiwa kulipa kwa awamu na hii ni mahususi ili kuwapunguzia wazazi mzigo.

Wote mnakaribishwa, mlete mwanao leo ufaidi matunda ya uwekezaji wako katika elimu.

Kwa mawasiliano zaidi piga Phone: DIRECTOR – 0754027426 | MANAGER – 0752205252 | HEAD TEACHER – 0744814427

Mshirikishe na mwingine upatapo taarifa hii.